Thursday , 6th Aug , 2020

Chama Cha NCCR- MAGEUZI kimesema kuwa kipo tayari kushirikiana na Chama chochote chenye mlengo wa kidemokrasia katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.

Mkuu wa kitengo Cha mawasiliano na Uenezi wa NCCR Edward Simbeye

Akizungumza na wanahabari katika ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo Cha mawasiliano na Uenezi Edward Simbeye amesema kuwa kesho Agosti 7, 2020 wataanza vikao vya Mkutano Mkuu ambao utapitisha majina ya wagombea Kiti Cha Urais Tanzania bara na Zanzibar.

"Chama chetu kipo tayari kushirikiana na yeyote mwenye mlengo wa kidemokrasia, aliye tayari milango iko wazi", amesema Simbeye.

Aidha ameeleza kuwa wagombea waliojitokeza katika nafasi ya Urais ni wa nne upande wa Tanzania na mmoja Zanzibar huku waliotangaza Nia Ubunge wamefika mia mbili.