Saturday , 8th Aug , 2020

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeona kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii na kuibua taharuki kwa mashabiki wa sokahapa nchini.

Winga Benard Morrison akisaini mkataba wa kuitumikia Klabu ya Simba

Uongozi unafuatilia kwa karibu na umakini mkubwa suala hilo na ikithibitika hatua kali na za mfano zitachukuliwa kwa pande zote zinazohusika.

Aidha Uongozi unawataka wanachama na wapenzi wa Yanga kuwa watulivu kwani mchezaji Benard Morrison ana mkataba na Klabu hiyo hadi 2022 na shauri baina yake na Klabu bado liko mikononi mwa Shirikisho la Soka Tanzania na Jumatatu linaendelea kusikilizwa.