Saturday , 8th Aug , 2020

Klabu ya Bayern Munich itaikaribisha Chelsea kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora huku wakijivunia akiba ya ushindi wa 3-0 walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza huko Stanford Bridge.

Beki wa Bayern Munich, David Alaba akimzunguka mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa UCL ambao The Bavarians iliwatandika The Blues kwa bao 3-0 uwanjani Stanford Bridge.

HALI ZA WACHEZAJI

Kiungo Ng'olo Kante na Rouben -Loftus Cheeck watarejea kikosini lakini Christian Pulisic,Pedro Rodrigues, Cezar Azpilicueta ambao walipata majeraha kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Arsenal .

Vilevile Willian Da Silva akiwa hajasafiri na na timu ikitajwa anakamilisha uhamisho wake wa kutua katika klabu ya Arsenal.

Wachezaji Marcos Alonso na Jorginho wote hawatokuwepo kutokana na kadi walizopata katika michezo ijayo.

Kwa upande wa Bayern Munich watawakosa nyota wake Kingsley Coman mwenye maumivu ya misuli ya paja,ingawa ndio nafasi pekee kwa Ivan Perisic kucheza,pia watamkosa Benjamin Pavard,hivyo ni nafasi kwa Joshua Kimmich kucheza kwenye idara ya kiungo.

.ALICHOSEMA KOCHA WA CHELSEA.

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amesema kikosi chake kina nafasi ya kufanya jambo kubwa la pekee dhidi ya Bayern Munich leo.

MWENENDO WA TIMU HIZI ZIPOJE?

Katika mechi 7 za mwisho za Chelsea za ugenini, hawajapata ushindi hata mechi moja huku Bayern Munich imeshinda mechi 17 mfululizo za mashindano yote za hivi karibuni.