
Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Amesema hayo akiwa anazungumza na wanachama na wananchi wa Zanzibar mara baada ya kupokelewa kutoka bandarini akiwa ameongozana na mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Membe na mgombea mwenza Prof Omar Hamad na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
"Kwanza kabla sijasema lolote naomba kuweka wazi, tumekusanyika hapa si kwa mkutano wa kampeni ,kampeni bado tunajua kwa upande wa Zanzibar kampe zinaanza tarehe Septemba 11 tunakuwa na siku 45 za kufanya kampeni", amesema Maalim Seif.
Aidha Maalim Seif ameongeza kuwa, “Naomba niwashukuruni nyote ambao tangu alafajiri leo mmesubiri wagombea kwa hamu kubwa hata chai hamkunywa, lakini kwasababu ya mapenzi ya kweli kwa chama chetu na wagombea wetu mmekubali mbaki ilimuwasalimu na kuwakaribisha hapa Zanzibar”.
Leo Wagombea wa urais kupitia chama hiko kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara waliwasili Zanzibar huku msafara wao ukipokelewa na mafuriko ya watu waliokuwa Bandarini wakiwasubiri kuwalaki, ambapo waliongozana na msafara huo hadi kwenye ofisi za chama hicho zilizopo huko Vungi.