
Kauli hiyo imetolewa na Rais huyo kwenye Mkutano wa Bodi ya Ligi na Viongozi wa Timu unaofanyika kwenye Ofisi zilizopo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Karia ameongeza kwamba kumekua na kelele zinazodai kwamba TFF inaingilia maamuzi ya Bodi ya Ligi jambo ambalo halina mashiko.
Aidha Rais Karia amewataka baadhi ya Viongozi kuacha kuwatuma wasemaji wa Vilabu vyao ambao ndio wamekua mstari wa mbele kuongea mambo yasiyofaa katika soka.
Jambo jingine la kushangaza viongozi wa Klabu za Simba na Mtibwa Sugar hawakutokea kwenye kikao hiko chenye kusudio la kufanya tathmini ya msimu uliomalizika na mkakati wa kuanza msimu ujao.