Rais Magufuli wakati akikabidhiwa Tuzo na Askofu wa Kanisa la TAG Dkt Barnabas Mtokambali.
Tuzo hiyo amekabidhiwa leo Agosti 14, 2020, na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt Barnabas Mtokambali, katika Mkutano Mkuu wa Baraza kuu la Kanisa la TAG, wakati akifungua mkutano huo, uliofanyika Jijini Dodoma.
Aidha Askofu Mtokambali amesema kuwa jambo lililofanywa na Rais Magufuli katika kipindi kile la kuruhusu shughuli za kimaendeleo ziendelee kama kawaida, lilikuwa la tofauti kwani ni katika kipindi hiko ambapo Mataifa mengine yaliweka nguvu yakuzuia watu wasitoke majumbani.





