Friday , 14th Aug , 2020

Msanii wa BongoFleva Mr Blue ameshea stori kadhaa kuhusiana na maisha yake ya muziki, shule, familia na magumu aliyopitia hadi kuifikia hapo alipo sasa hivi.

Msanii Mr Blue kutoka upande wa kulia, kati mtangazaji Dullah Planet na kulia ni Lesa Sidi

Akieleza hayo kupitia  "Wiki ya Blue" ya kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Mr Blue amesema wakati anaanza muziki jina lake lilikuwa kubwa kuliko uhalisia wake, na pesa ya kwanza kupokea ni Milioni 1 ambazo alizificha kwenye nguo ya ndani.

"Album yangu ya kwanza ilikuwa ni muziki na shule, tena nilikuwa darasa la 6 nikiwa na miaka 14, tukakubaliana na G Love kuhusu malipo, pesa yangu ya kwanza ilikuwa ni Milioni 1 nikaiweka kwenye nguo za ndani kwa sababu zile pesa zilikuwa nyingi hasa kwa mwaka 2003 kwani maisha yangu yalikuwa ya hali ya chini kwa hiyo ile pesa ilikuwa kubwa sana" ameeleza Mr Blue 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.