Saturday , 15th Aug , 2020

Precious Stellah maarufu kama Beyonce wa Buza, ambaye alijulikana baada ya kuvuliwa wigi na mchekeshaji Ebitoke wakati wanagombana amesema anampango wa kuwarudisha na kuwasimamia wasanii wa zamani kama TID na Q Chief.

Msanii TID na Precious Stellah "Beyonce wa Buza"

Akipiga stori mbele ya kamera za EATV & EA Radio Digital, Beyonce wa Buza amesema TID hana pesa kwa sasa ila ana kipaji kikubwa hivyo anataka kumsadia ili aache kulalamika na vitu kama anaibiwa misemo.

"Tunataka kuwarudisha wasanii wa zamani kama TID na Q Chief, TID yeye analalamika ameibiwa msemo wake mimi naona ni upuuzi tu atufuate sisi ambao tuna pesa tumsaidie, TID pesa hana kwake hiyo changamoto kama kipaji anacho na kuimba anajua, ningependa anitafute ili tuweze kumsaidia na kumsaini" amesema Beyonce wa Buza 

Zaidi tazama kwenye video hapa chini.