Tuesday , 18th Aug , 2020

Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya inachezwa usiku wa leo Agosti 18, 2020, katika Dimba la Estadio da Luz nchini Ureno. Ambapo RB Leipzig ya Ujerumani watamenyana na PSG ya Ufaransa.

Neymar Jr na Kylian Mbappe

RB Leipzig kwa mara ya kwanza wanacheza katika hatua hii ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya Uefa Champions League katika historia ya klabu hiyo. RB Leipzig wametinga katika hatua hii baada ya kuifunga  Atletico Madrid ya Hispnaia mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainal.

Ushindi wa jioni wa mabao 2-1 dhidi ya Atalanta ambao waliupata PSG ulitosha kuipa PSG tiketi ya kucheza  nusu fainali ya michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 25. Mara ya mwisho kucheza katika hatua hii ilikuwa msimu wa 1994-1995 ambapo walitolewa na AC Milan ya Italia.

Ibrahim Konote ndio mchezaji pekee mwenye majeruhi kwenye kikosi cha RB Leipzig na ataukosa mchezo wa usiku wa leo na kocha Julian Nagelsmann anaweza rejea na kikosi kilekile kilicho cheza  kwenye mchezo wa Robo fainali dhidi ya Atletico Madridi.

Kocha ThomasTuchel wa PSG ataendelea kuikosa huduma ya kiungo Marco Verrati mwenye majeruhi lakini pia goli kipa namba moja Keylor Navas ambaye aliumia kwenye mchezo wa Robo fainali dhidi ya Atalanta na kipa namba mbili Sergio Rico ataanza katika mchezo wa leo.

Wachezaji wa RB Leipzig

Ángel Di María anarejea pia kwenye kikosi cha PSG baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Atalanta kutoka na adhabu na Kylian Mbappé anaweza kuanza katika mchezo huu baada ya kucheza dakika 30 kwenye mchezo wa robo fainali.

Vikosi vinavyoweza kuanza katika mchezo wa leo kwa timu zote mbili.

RB Leipzig: Gulacsi, Klostermann, Upamecano, Halstenberg, Angelino; Laimer, Kampl; Sabitzer, Olmo, Nkunku; Poulsen

PSG : Rico, Kehrer, Silva, Kimpembe, Bernat; Di Maria, Paredes, Marquinhos, Neymar, Mbappe, Icardi