Thursday , 20th Aug , 2020

Mshambuliaji chipukizi wa timu ya Barcelona, Ansu Fati ametangaza kubadilisha wakala wake ghafla na sasa atakua chini ya Jorge Mendes huku akiachana na Rodrigo ambaye ndiye anayefanya kazi na Lionel Messi.

Ansu Fati akiwa uwanjani katika moja ya mechi za Barcelona

Jorge Mendes  ambaye ni wakala maarufu zaidi wa wachezaji duniani ambaye anamsimamia mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo.

Wadadisi wa mambo wanatia mashaka makubwa wa Fati kuendelea kusalia katika timu ya Barcelona kwa kuwa wakala huyu ni  mtalamu sana wa kupambania masoko bora ya  wateja  wake ndani ya na nje ya Barcelona (Mendes anazingatia zaidi fedha kuliko kitu chochote).

Fati ambaye kiasili ni mzaliwa wa  Guinea Bissau barani Africa lakini aliwafuata wazazi wake nchini Hispania na baadaye alijiunga na Barcelona  ya vijana  kisha akapandishwa  kikosi cha wakubwa.