
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera
Hayo yamesemwa leo Agosti 26,2020, na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera na kusema Tume inashirikiana na umma ili kuhakikisha uchaguzi huu unakuwa wa huru na haki.
"Mtu ukiona hujateuliwa ni vizuri uulize kwa msimamizi wa uchaguzi akuelezee yeye ni kwanini na sisi Tume tuko tayari kushirikiana na nyinyi ili kuhakikisha uchaguzi huu unakuwa wa huru na wa haki " amesema Dkt Mahera.
Aidha Tume ya uchaguzi imesema kuwa inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, hivyo kama mgombea hajateuliwa ni kwasababu hajatekeleza masharti yaliyowekwa na tume kwa kila ngazi.
"Huwezi ukakata mtu kwa matakwa yako kwa sababu Tume ya Taifa inafanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni, tumeweka sifa za wagombea kwa ngazi zote, Madiwani, Wabunge na Rais, lakini tumeweka masharti ya uteuzi, mtu ukimuona hajateuliwa maanake hajatekeleza yale masharti" ameongeza.