
Staa wa Milwaukee Bucks, Giannis Atetokounmpo akionyesha ubora wake katika moja ya mchezo wa NBA.
Wakiongozwa na mlinzi wao Sterling Brown,wachezaji wa Bucks waliingia uwanjani lakini hawakucheza bali walituma ujumbe unaoshinikiza uhitaji wa haki kwa mtu mweusi na walisisitiza kwa jana isingekua rahisi kwao kucheza mchezo wao.
Baada ya Bucks kugomea mchezo huo,timu za Huston Rockets,Oklahoma City Thunder ambazo pia zilitarajiwa kucheza mchezo wao wa tano ziliunga mkono jitihada za Milwaukee Bucks vilevile mchezo mwingine ulioahirishwa kati ya Los Angeles Lakers dhidi ya Portland Trail Blazers .
Timu za Los Angeles Clippers na Los Angeles Lakers ambazo ndio zinapewa nafasi ya kutwaa ubingwa lakini wao wametangaza kuwa hawatocheza iwapo hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wanaokiuka haki za watu weusi.
Ni Boston Celtics na Toronto Raptors pekee ambazo kwa mujibu wa ratiba zilipaswa kucheza leo,ndizo timu pekee ambazo hazijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo la kikatili
Ikumbukwe miezi minne iliyopita Jeshi la Polisi Nchini Marekani lilimuua George Floyd jambo lililoleta taharuki kubwa na hata wanamichezo mbali mbali Dunani kote
(MLS)-LIGI YA MPIRA WA MIGUU NAO WATUMA UJUMBE
Wakati NBA ikisimama,Mchezo wa mpira wa miguu Nchini Marekani kati ya Inter Miami dhdi ya Atlanta United nayo haikuchezwa ingawa wachezaji waliingia Uwanjani na kukusanyika kwa pamoja wakituma ujumbe wa umoja katika kupigania haki na usawa nchini Marekani.
Ukiachana na soka,michezo ya Tenis,Baseball,na mpira wa magongo (Baseball) nayo imeahirishwa ikiwa ni katika harakati hizo hizo za kupigania haki ya mtu mweusi.
KINACHOSEMWA NA WATU WENYE USHAWISHI
LeBron James ambaye ni Staa wa Los Angeles Lakers ameandika,''Nina watoto wawili wa kuwazaa,wanaishi hapa Marekani,na kila kinachotoea sasa juu ya ukatili wa Jeshi la Polisi dhidi ya watu ambao ni familia yangu napata mashaka makubwa sana''
Barack Obama ambaye ni Rais wa zamani wa Marekani ameandika''Niliwaambia wachezaji wa Bucks kusimamia wanachokiani,kocha DocRivers pamoja na NBA pia WNBA wamekua mfano mzuri,itasaidia taasisi zote kusimamia thamani yetu''
HATUA IPI INAFUATA?
-Baada ya mgomo huo wa wanamichezo nchini Marekani, kwa pamoja wachezaji hao wameungana na sasa watafanya kikao na Taasisi ya ''African American Community'' kujadili namna ambavyo watafikisha mashtaka yao ngazi za juu ili kujua hatma ya matukio haya ya ukiukwaji wa haki ya mtu mweusi.
-Kwa upande kwa mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa(National Basekatball Players Association), Chriss Paul ambaye ni mchezaji wa Oklahoma City Thunder atakutana na Uongozi wa (National Basketball Association )ili kujadili mustakabali wa ligi yao.
ATHARI ZA MGOMO HUO.
Iwapo Lakers na Clippers zitagomea moja kwa moja kushiriki ligi ya NBA, zitapunguzo mvuto kwa watazamaji na hata kwa makampuni ya kibiashara ambayo yanawekeza kwenye mchezo huo ikizingatiwa Timu hizo mbili ndizo zenye ushawishi mkubwa kutokana na aina ya wachezaji walionao mfano kwa Lakers wanae LeBron James na hata Antony Davis huku Clippers ina mastaa kama Kehwi Leonard na Paul George.