
Kocha mpya wa Yanga Zlatko Krmpotic alipowasili Tanzania
Yanga imemtangaza kocha huyo kufuatia kutowasili kwa kocha ambaye aliingia mkataba na klabu hiyo awali, Cedric Kaze raia wa Burundi ambaye alitoa udhuru utakaomfanya kuchelewa kuripoti kwenye klabu.
Kocha Zlatko ni mzoefu wa kufundisha klabu mbalimbali za Afrika, akiwa amefundisha jumla ya klabu tano ikiwemo, Zesco United, Jwaneng, Royal Eagles, APR FC na Polokwane City ambayo ameifundisha msimu uliopita.
Lakini kocha huyo amekuwa na rekodi ya kutodumu kwa muda mrefu na timu eidha kwa kutofanya vizuri au kushindwana na uongozi wa klabu husika, ambapo katika klabu mbalimbali ambazo amezifundisha barani Afrika ni klabu ya Jwaneng pekee ambayo amedumu kwa muda mrefu ambazo ni siku 189.