Sunday , 30th Aug , 2020

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kamwe hatosita kufuta serikali za vijiji ambazo zitashindwa kutatua au kuwa sehemu ya migogoro.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo

Ndikilo amesema hayo alipokuwa katika ziara yake wilayani Rufiji mkoani Pwani Agosti 29, 2020.

''Nitafuta serikali za vijini na kuwafuta kazini watendaji wa vijiji wanaochochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji mkoani kwetu'', alisema Ndikilo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo alipata fursa ya kukagua daraja la Mkapa lililopo wilayani Rufiji ikiwa ni agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa wakati akitokea katika mazishi ya Rais wa awamu ya tatu marehemu Benjamin Mkapa.

Rais alimuagiza mkuu wa mkoa kuhakikisha taa zilipo katika daraja hilo zinawaka ikiwemo kujenga kibanda cha walinzi katika daraja hilo ambacho tayari kimeshakamilika.