
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Tundu Antipas Lissu
Amesema katika siku 100 za kwanza baada ya kupata ushindi katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, ataunda tume kwa ajili ya upatanishi na ukweli ili kuvumbua mabaya yanayofanyika katika nchi.
‘‘Nikiingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu katika siku 100 za kwanza nitaunda Tume ya upatanishi na ukweli ili tufahamu mambo yote haya mabaya ambayo yamefanyika katika nchi yetu, tuwafahamu walioyatenda, tufahamu kwanini waliyatenda, nani aliyewatuma halafu tuwaambie tubuni dhambi zenu’’ amesema Lissu.
Aidha Mgombea huyo amedai kuwa lengo sio kulipa kisasi bali wanataka kufahamu ukweli ambao utawaweka huru.