
Dkt John Pombe Magufuli
Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 14, 2020, wakati wa mkutano wake wa kampeni Chato mkoani Geita, ambapo ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano imejikita katika kutekeleza miradi ambayo itasisimua uchumi ili kuchagiza maendeleo ya nchi pamoja na kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
''Tunaitengeneza nchi kuwa ya kisasa, ndiyo maana tunawaomba wananchi watupe miaka mingie mitano, unapotaka kujenga uchumi wa nchi yoyote lazima ujenge uchumi wa watu walio na afya njema na ndiyo maana katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka huu, tunataka bima ya afya ichukue watu wote'', amesema Dkt Magufuli.
Aidha Dkt Magufuli ameongeza kuwa, "Uongozi ni kutoa sadaka, nimeamua kutoa maisha yangu ya uongozi kama sadaka kwa Watanzania, hii kazi ndugu zangu ni ngumu lakini ninaweza kuifanya tena kwa miaka mitano".