Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari
Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 16, 2020, na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari, ambapo amesema kuwa tamko hilo linakuja baada baada ya Serikali ya Kenya kuiondolea Tanzania vikwazo vya raia wake kuingia humo bila kuwekwa karanyini.
Aidha Mkurugenzi huyo ameyataja mashirika ya Ndege ya Kenya yaliyoruhusiwa kuendelea na shughuli zake kuwa ni Kenya Airways, Fly 540 Limited, Safarilink Aviation na AirKenya Express Limited.
Jana Septemba 15, 2020, nchi ya Kenya ilitoa orodha ya nchi 147 ambazo raia wake wataingia nchini humo bila kuwekwa karantini na katika nchi hizo Tanzania iliorodheshwa.