Wakazi wa Geita wakifanya usafi
Afisa mazingira wa halmashauri ya mji wa Geita, Albert Auson amesema kuwa mwananchi yeyote atakayeenda kinyume na hapo ataadhibiwa kwa kufuata sheria ya usafi na mazingira ambapo atakayekamatwa atalipa faini kuanzia laki mbili hadi milioni moja au kwenda jela miezi 24 au vyote kwa pamoja.
Kwa upande wa wakazi wa mkoa huo wamesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kupunguza magonjwa ya mlipuko ambapo pia wamewatahadharisha wale wote ambao watakuwa wachafuzi wa mazingira kuwa sheria itachukua mkondo wake.
"Wengi wametelekeza maeneo kama haya ya hifadhi ya barabara na kuiachia manispaa ifenye usafi jambo ambalo si sahii mana hata manispaa kuna baadhi ya maeneo wanashindwa kufika,kila raia ambaye amezungukwa na maeneo ambayo ni machafu anapaswa kusafisha kwani mazingira ukiyatunza na yenyewe yanakutunza’’, amesema Jonathan James.