
Job Ndugai
Ndugai ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 21, 2020, katika mkutano wa kampeni za CCM, wakati akimuombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Urambo Mama Margareth Sitta.
"Sisi wa CCM tunaomba kura tatu ya kwanza ya Rais, wabunge na madiwani na hapa Urambo namuombea Mama Margareth Sitta na ukipiga kura kwa Magufuli na Mama Sitta kwa Urambo hapa unapata 'bonus' kwa sababu mtampata mbunge wa Viti Maalum anaitwa Jackline", amesema Spika Ndugai.
Aidha Ndugai ameongeza kuwa, "Tusichague wapinzani kwa sababu tatizo lao ni kupinga kila kitu, Rais Magufuli akitaka kujenga reli wanapinga, akitaka kujenga barabara na kusambaza umeme na akitaka kutoa maji Ziwa Victoria kuleta Urambo wanapinga sasa mtu wa namna hiyo wa nini".