
Mgombea mwenza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu
Samia Suluhu amesema hayo leo Oktoba, 11, katika viwanja vya Muze Sumbawanga, Mkoani Rukwa, katika muendelezo wa kampeni zake nakuongeza kuwa watoto wa kike wakisikilizwa inawajengea mazingira bora ya baadae.
"Kimataifa leo ni siku ya mtoto wa kike,tunachokisema hapa mtoto wa kike anahaki ya kupewa nafasi,kupata matibabu,kusikilizwa matakwa ya moyo wake kama mtoto wa kiume’’Samia Suluhu
Pia mgombea mwenza huyo ameendelea kunadi sera za chama chake ambapo ameahidi kushughulikia changamoto ya barabara na pindi ujenzi utakapokamilika utasaidia kuimarisha uchumi pamoja na kusaidia sekta ya usafiri na usafirishaji
"Napenda niwape taarifa ya faraja tunakwenda kuongeza uwezo wa TARURA kitaalamu lakini pia kifedha ili waweze kushughulikia barabara zinazowahusu tunajua ni taasisi tumepanga kwenda kuiimarisha’’Samia Suluhu
Aidha katika kuadhimisha siku hii East Africa Tv, na East Africa Radio, wamefanya matembezi ya hisani katika wilaya ya Kisarawe wakiungana na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, lengo ikiwa ni kumbakiza mtoto wa kike shuleni kwa kumpatia taulo za kike.