
Mgombea urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, akisalimiana na wananchi mkoani Tabora.
Akizungumza hii leo Oktoba 12,2020, katika kampeni zake zilizofanyika Nzega, mkoani Tabora, amesema kuwa ili wananchi hao wapate maendeleo ya uhuru na haki inawapasa kuchagua chama hicho kiingie madarakani ili waweze kupata maendeleo.
''Tujenge nchi ya watu ,huwaliohururu kusema na kuendesha maisha yao bila kubugudhiwa na kutenda haki kwa kila mmoja wetu'' amesema Tundu Lissu.
''Kwenye uchaguzi mkuu huu chagueni baraza la madiwani litakaloongozwa na CHADEMA, kwa sababu kwenye halmashauri ni muhimu hela za maendeleo yenu wekeni kwenye halmashauri ya CHADEMA ili mambo yaende''ameongeza.
Aidha amesema kuwa wilaya ya Nzega imebarikiwa na madini ambapo amewataka wananchi kumchagua ili waweze kuleta maendeleo yenye tija kwao.