
Mgombea Urais Zanzibar, kwa tiketi ya chama cha Act-Wazalendo Maalim Seif Hamad
Akizungumza leo, katika muendelezo wa kampeni zake zilizofanyika Jadida Pemba,mgombea huyo ameahidi kurejesha mamlaka kamili ya wazanzibari ili waweze kufanya wanayoyataka.
''Tukiwa na mamlaka yetu kamili tutafanya mambo yetu yote tunayoyataka wala tabia ya maamuzi kutolewa Dodoma tarehe 29 ndio mwisho'' amesema Maalim Seif
Aidha mgombea huyo amewataka vijana pamoja na wananchi wote kwa ujumla kumchagua ili waweze kudai haki ya nchi yao.