Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Arusha, Sirro amewaambia wananchi kuwa askari wamejipanga kuhakikisha wanasimamia amani na haki.
“Arusha ni mahala ambapo miaka ya nyuma kulitokea fujo kwahiyo ni mahala ambapo tumepanga, tumeweka askari wa kutosha, askari wa kirai, wa operesheni na askari wa upepelezi wote wapo timamu kuhakikisha arusha inakuwa shwari” amesema IGP Sirro
Aidha IGP Sirro ametoa tahadhari kwa vikundi mkoani humo ambavyo vinataka kuleta uvunjifu wa amani kulekea uchaguzi mkuu, “Nina taarifa kuna vikundi vichache vinataka kuleta uvunjifu wa amani wasijaribu kufanya hivyo wakifanya hivyo maana yake wanajiingiza kwenye kutenda makosa natutawashugulikia kabla ya siku yenyewe” amesema IGP Sirro