Sunday , 1st Nov , 2020

Najua umeshaisikia ile kauli inayosema kabila la Wakinga kutokea Mkoani Njombe wamefanikiwa sana kwenye biashara ya maduka kule Kariakoo, na inasemekana sababu za kufanikiwa kwao ni kuhusishwa na masuala ya imani za kishirina kama uchawi.

Msanii na mfanyabiashara Shilole

Sasa huyu hapa n msanii Shilole ametolea ufafanuzi kuhusu hilo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshea 'experience' yake baada ya kutembelea sehemu za biashara za kabila hilo ambapo ameeleza kuwa 

"Mimi pia nimewahi kusikia hiyo kauli, nilivyo mpana nikasema ngoja niende huko Kariakoo nikaone hao Wakinga nieleweni vizuri, sikufuata uchawi, lengo ilikuwa kuona wanafanyaje biashara maana mimi kwa ninavyofahamu, utajiri unaletwa na kazi

Aidha Shilole ameongeza kuwa "Kifupi wengi wa hao wanaoitwa wachawi wa Kikinga, hawajui hata sura ya tunguli, uchawi wao ni wanafanya kazi sana, wanajitoa kwenye biashara zao, wametumwa hela hivyo wanazitafuta na kuzitunza kwa nidhamu kubwa, mtu wa namna hiyo mafanikio yako wazi mbele yake, uchawi ni kazi, nidhamu ya fedha na kujitoa kusiko kwa kawaida kwenye kazi zetu"