Monday , 2nd Nov , 2020

Kocha wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda amesema kuondokewa na baadhi ya wachezaji muhimu ndio sababu kuu ya wao kuanza kwa kusuwasuwa msimu huu.

Kocha wa Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda (Pichani) akiingia kwenye uwanja wa mazoezi.

Mgunda ameyasema hayo kufuatia jana kikosi chake kupokea kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa Ruvu Shooting katika mchezo wao wa tisa wa ligi kuu ya Tanzania bara.

''Kwakweli wachezaji wetu wengi walikoua wameunda msingi katika timu wameondoka mfano Bakari Mwamnyeto ameenda Yanga, Ibrahim Ame kaenda Simba, Ayoub Lyanga kaenda Azam, unaona ni jinsi gani timu kama yetu kupoteza wachezaji kama hawa ni tatizo hilo''.

Coastal Union imeshapoteza mechi 5 kati ya 9 huku ikishinda mechi 2 pekee na sare 3, sasa ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 9 .