
Kushoto Mgombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Republic Donald Trump na Kulia ni mgombea wa urais wa Chama cha Democratic Joe Biden
Wagombea hao wawili wanalenga kuonyesha tofauti wakati ambao nchi ya marekani imekumbwa na janga la corona ambapo hadi sasa wamarekani zaidi ya milioni 93 wameshapiga kura za awali.
Kila upande unasisitiza kuwa uko karibu na ushindi kutokana na muitikio wa watu waliojitokeza katika upigaji kura za awali huku mgombea wa Chama cha Demokratic Joe Biden akieleka kuwa na uwezekano wakuwapata wajumbe wa kumpigia kura zaidi.
Wamarekani wanajitayarisha kupiga kura hapo kesho kwa ajili ya kumchagua rais mpya ambapo Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Donald Trump wa chama cha Republic akitetea kiti hiko huku akichuana na mpinzania wake Joe Biden ilihali, watu zaidi ya 230,000 wameshakufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.