
Mkurugenzi wa ufundi wa Gwambina, Mwinyi Zahera(Pichani) akizungumza na EATV.
Zahera ambaye alitimuliwa mapema msimu uliopita, amesema mpira unabadilika na hata wachezaji pia, alivyokuwepo Yanga ilikuwa na wachezaji tofauti na mazingira pia, hivi sasa wanajipanga kwa ubora wao na sio zamani.
''Yanga ni tofauti na kipindi nilichokuwepo kwakuwa hata mazingira yamebadilika, hivyo kwasasa tutawakabili kutokana na ufanisi walionao hivi sasa'' alisema Zahera.
Yanga ambayo iwapo itashinda leo itakamata usukani wa VPL kwa kufikisha alama 25 wanahitaji kuendeleza ushindi wa asilimia 100 kabla ya kukutana na watani wao Simba, huku Gwambina wanahitaji kushinda ili kujisogeza juu ya msimamo wa ligi.