
Kikosi cha Yanga SC
Gwambina FC watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani (Gwambina Complex), watakuwa wenyeji wa Yanga SC. Timu hizi zinashuka dimbani jioni ya leo zikiwa zinatofautiana kwa alama 13 kwenye msimamo wa ligi. Yanga wamekusanya alama 22 mpaka sasa katika michezo 8 na wapo nafasi ya 2, wakati Gwambina wapo nafasi ya 14 wakiwa na alama 9 katika michezo 9.
Ni mara ya kwanza timu hizi zinakutana katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara, hivyo huu ni mchezo wa kihistoria kwa timu zote mbili hususani Gwambina ambao huu ni msimu wao wa kwanza kwenye ligi kuu. Ingawa msimu uliopita timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa kombe la FA hatua ya 16 bora na Yanga walishinda bao 1-0.
Gwambina wanaingia katika mchezo huu wakiwa hawajashinda mchezo hata 1 kwenye michezo 3 ya mwisho ya ligi, wakati Yanga wameshinda michezo 7 mfululizo na endapo kama watashinda mchezo wa leo, utawafanya wakamate usukani kwenye msimamo wa ligi.
Kikosi cha Gwambina FC
Mchezo mwingine unachezwa mkoani Mara uwanja wa Karume, ambapo Biashara United wataminyana na timu ya manispaa ya Kinondoni, KMC FC.
Msimu uliopita katika uwanja wao wa nyumbani Biashara, waliifunga KMC mabao 4-0, na wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao wa kwanza katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Yanga kwa bao 1-0, na ndio mchezo pekee waliopoteza nyumbani kwenye michezo 5 msimu huu.
Ushindi wa goli 3-0 walioupata KMC dhidi ya Gwambina kwenye mchezo uliopita ndio ushindi pekee walioupata kwenye michezo 6 ya mwisho ya ligi, Biashara United wapo nafasi ya 4 wakiwa na alama 16 ni tofauti ya alama 2 tu na KMC wenye alama 14 walio nafasi ya 6.
Ratiba ya michezo ya raundi ya 10
Jumatano Novemba 4
Simba SC Vs Kagera Sugar
Namungo FC Vs JKT Tanzania
Mwadui FC Vs Ruvu Shooting
Alhamisi Novemba 5
Mbeya City Vs Polisi Tanzania