Tuesday , 3rd Nov , 2020

Bodi ya ligi Tanzania (TPBL) imefanya mabadiliko ya ghafla kwenye ratiba ya mchezo mmoja, ambapo mabadiliko hayo yameonesha kuziumiza baadhi ya timu.

Timu ya Ruvu shooting ambayo imebadilishiwa ratiba ya mchezo wake dhidi ya Mwadui

Kwa mfano timu ya Ruvu Shooting iliyopaswa kucheza na Mwadui ya Shinyanga tarehe 07/11/2020, kwenye ratiba ya awali ghafla wakapewa taarifa mechi yao kuchezwa Jumatano tarehe 4/11/2020 .hivyo wakalazimika kuanza safari saa 5:00 asubuhi siku ya Jumanne kwa njia ya barabara

Bodi ya ligi inayoongozwa na Mwenyekiti wake Steven Mguto, imekuwa kwenye lawama za mara kwa mara juu ya mabadiliko ya ratiba katika ligi madaraja yote wanayo simamia

Uteuzi wa Almas Kasongo kushika nafasi ya mtendaji mkuu wa bodi hiyo, kulileta imani kubwa ya kutatua tatizo la ''pangapangua'' za mara kwa mara kutokana ma uzoefu na uweledi wake katika mchezo wa soka

Ikimbukwe kuwa hata mchezo mkubwa wa ligi ya Tanzania, inayohusisha Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi tarehe 7 uwanja wa kumbukumbu ya Hayati Benjamin Mkapa, awali ulipaswa kuchezwa Oktoba 18, lakini ukaahirisha na sasa unategemewa kuchezwa Jumamosi hii.