Wednesday , 4th Nov , 2020

Kuelekea kilele cha Uchaguzi nchini Marekani ambapo Marekani imekuwa ikisaidia nchi za Kiafrika katika masuala ya kukuza demokrasia na maendeleo, nchi za kiafrika zinapaswa kujifunza kuwa na demokrasia iliyokomaa na yenye uwazi.

Kushoto mgombea urais wa chama cha Republic Donald Trump na Kulia mgombea urais chama cha Democratic Joe Biden

Akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast, mchambuzi wa siasa za kimataifa Mbwana Allyamtu, amesema uchaguzi wa Marekani umefuata mfumo wa utaratibu wa uchaguzi ulioasisiwa tangu miaka 200 iliyopita ambao umelenga kulinda muungano wa taifa hilo.

“Kitu kikubwa chakujifunza Afrika au nchi nyingi zinazomtazama Marekani kuwa na demokrasia iliyokomaa japo atuwezi kuiga mambo yote ikiwemo utaratibu na tamaduni zake, demokrasia ya wazi ambayo haimtengi mtu yeyote, yule aliye madarakani au anayetafuta kiti cha kuingia madarakani” amesema Mbwana Allyamtu

Akizungumzia suala la mgombea yupi anayeungwa mkono na nchi za Afrika alikuwa na haya yakusema, “Wamarekani wengi na asilimia kubwa ya mataifa makubwa duniani , nchi nyingi za Afrika zinamuunga mkono Joe Biden kwasababu ya sera ambazo zimewaumiza kwa Trump ,sera za mambo ya nje” amesema Mbwana Allyamtu

Aidha Mbwana amesema kuwa uchaguzi huu ni mgumu kuutabiri na mwepesi kuutabiri kutokana na mfumo wa upigaji kura kuwa mgumu huku akidai kuwa muda wowote mambo yanaweza kubadilika.