Wednesday , 11th Nov , 2020

Wanafunzi wa Kisiwa cha Izumacheki kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Geita, mkoani Geita, wanalazimika kuvuka maji kwa kutumia mitumbwi inayosafiri kwa muda wa nusu saa kwenda shuleni, Kata ya Nkome, kutokana na eneo wanaloishi kutokuwa na shule, kitendo kinachohatarisha usalama wao.

Baadhi ya wananchi wakipanda mtumbwi.

Hali ya ukosefu wa shule ya sekondari katika kisiwa hicho, imesababisha mkuu wa wilaya ya Geita, Fadhili Juma, kutembelea katika maeneo hayo na kuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuweka mikakati ya ujenzi wa shule ya sekondari, ili kuondoa changamoto inayowakabili wanafunzi hao.

"Halmashauri yangu ninaiagiza ianze mpango wa ujenzi wa sekondari, kwa sababu ni 'risk' kwa watoto kupanda boti kila siku kwenda kutafuta elimu kwenye Kata jirani na mpango wa serikali hii ni kuwa na sekondari katika kila Kata", amesema DC Juma.

Tazama video hapa chini.