Thursday , 12th Nov , 2020

Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imekamilisha usajili wa mshambuliaji Makusu Mundele kutoka AS Vita ya Congo kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Makusu Mundele akiwa katika mkutano na waandishi wa habari

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akihusishwa na klabu ya Yanga ya Tanzania, amesema amefurahi kujiunga na miamba hiyo ya Afrika ambayo inahistoria nzuri katika michuano ya vilabu.

Mundele ambaye aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji, Misri, Algeria na Hungary, anategemewa kuisaidia Pirates katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika msimu huu.