
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Profesa Kabudi, ametoa kauli hiyo hii leo Novemba 16, 2020, wakati akizungumza mara baada ya kuapishwa kutumikia nafasi hiyo kwa awamu ya pili sasa.
"Mh. Rais hii ni mara ya nne unanipa mshituko nisioutarajia, unanipa nafasi bila mimi kutarajia na umeniacha na butwaa, Januari 16, 2017 saa 10:00 jioni nikiwa darasani nawafundisha wanafunzi sheria kupitia kwa Msigwa uliniteua kuwa mbunge", amesema Profesa Kabudi.
Aidha Profesa Kabudi ameongeza kuwa, "Nakumbuka wosia niliopewa na baba yangu, aliniambia, usiruhusu watu wakuandae kwa cheo chochote na wewe mwenyewe usijiandae kwa cheo chochote, ukiwaruhusu kama hawana mamlaka utafadhaika, na pia usijiandae kwa cheo chochote maana ukikipata utakuwa na kiburi na ukikikosa utamchukia yule aliyepewa na kumfanya adui yako"