
Taifa Stars wakiwa mazoezini kujiwinda na Tunisia
Katika wadau 10 wa mchezo wa soka waliohojiwa juu ya matokeo ya Taifa Stars dhidi ya Tunisia, 6 hadi 7 wameomesha imani ya kupata matokeo ya ushindi huku 3 hadi 4 wakionesha hofu na kupata matokeo alama yeyote ile.
Kwa mujibu wa tafiti, imani hiyo inatokana na matokeo ya awali katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa tarehe 13/11/2020 ambapo ulimalizika kwa Tunisia kupata ushindi wa bao 1-0, goli pekee lililotokana na penati iliyosababishwa na golikipa wa Taifa Stars Aishi Manula
Tunisia ambayo ipo kwenye nafasi ya 26 kidunia katika viwango vya soka vya FIFA na ya pili kwa bara la Africa, kwa sasa inaongoza kundi J ikiwa na alama 9 huku akifuatiwa na Equtorial Guinea yenye alama 6 ikifuatiwa na Libya na Tanzania zenye alama 3 kila moja lakini zikitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa