Monday , 23rd Nov , 2020

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Aboubakari Kunenge, amesema serikali inatambua changamoto wanazopambana nazo wauguzi hivyo itahakikisha inashirikiana nao kwa lengo la kuleta ufanisi katika kazi zao

 

Wa pili kulia Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Aboubakari Kunenge akisikiliza maelezo ya utendaji kazi kitengo cha dharura cha hospitali ya taifa ya Muhimbili

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam katika mkutano mkuu wa wauguzi wa mkoa huo wenye lengo la kujitathimini ili kupiga hatua zaidi kwenye utendaji wao

“Namuagiza Mganga Mkuu wa mkoa kuhakikisha mkutano wa wauguzi mkoa wa Dar es salaam uwe unafanyika tarehe kama ya leo kila mwaka” amesema Kunenge mkuu wa mkoa wa Dar es salaam

Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Dkt. Rashid Mfaume pamoja na muuguzi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Victoria Bura, kila mmoja kwa upande wake ameeleza changamoto na mafanikio kwa wauguzi