
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo
Hayo yamesemwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Morogoro mjini wakati akifungua mafunzo maalumu ya watumishi wanaotarajia kustaafu wapatao 223 kutoka makao makuu ya wizara , Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ,Vyuo vya Ualimu na Idara ya udhibiti wa shule ambao wapo chini ya wizara hiyo ambao ameahidi serikali itahakikisha michango ya watumishi waliopo chini ya wizara hiyo inawasilishwa kwa wakati kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
“Kwa sasa hivi tunahakikisha tunapitia kumbukumbu za kila mtumishi ili kuona mchango wa kila mwezi inaenda ,huko nyuma kulikuwa na tatizo kidogo palikuwepo na madeni ya ajabu ajabu , lakini hivi sasa mambo yamenyooka ni kutokana na mfumo uliowekwa “ alisema Dk. Akwilapo.
Aidha Dk Leonard Akwilapo amesema kuwa kwa kutunza kumbumkumbu kutasaidia watumishi wanapofikia umri wa kustaafu wapate mafao yanayostahiki kwa wakati ambayo yatawawezesha kushiriki shughuli za maendeleo ya kupitia miradi ya kiuchumi watakayoianzisha .
Dk. Akwilapo, aliwaagiza watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha wanapitia nyaraka zote za watumishi ili kuona mapungufu yanayojitokeza na kama kuna changamoto na ziweze kurekebishwa kabla ya kufikia Juni mwaka 2021 kwa lengo la kuzirekebisha kasoro hizo.