
Makamu wa Rais wa Geita Gold Mining (GGM), Simon Shayo
Akiwa hapo Simon Shayo, ameeleza kufurahishwa na mabadailiko ya teknolojia katika vyombo hivyo, ambayo ameeleza yatasaidia kuwafikia wadau wengi na jamii kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya ziara yake hiyo, amesema kuwa miaka 20 ya mafanikio ndani ya mgodi wa GGM, imesindikizwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari vya IPP Media.
Makamu wa Rais wa Geita Gold Mining (GGM), Simon Shayo ( wa pili kutoka kulia) na Meneja Mahusiano Stephen Mhando (wa kwanza kulia) wakipokea maelekezo mbalimbali kuhusu IPP Media.
“Tumeona mambo mengi ikiwemo mabadiliko makubwa kwenye teknolojia namna ya uandaaji wa habari na urushaji matangazo, na hii inatupa moyo nakutufariji kwasababu tunamtazama kama mdau wetu muhimu wa kuweza kufanya naye kazi ili tuweze kuwafikia wadau wengine”, amesema Shayo.
Aidha katika kuzungumzia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Shayo ametoa mtazamo wake kuhusiana na suala la unyanyasaji huku akiomba kila mtu kwenye jamii awe mlinzi wa mwenzake.
Makamu wa Rais wa Geita Gold Mining (GGM), Simon Shayo ( katikati) na Meneja Mahusiano Stephen Mhando (wa kwanza kushoto), wakiwa studio za ITV.
“Sisi tunaamini unyanyasaji wa aina yeyote, mtazamo wangu kuhusu hili, unyanyasaji wowote wa kijinsia ni uporaji na ni jambo ambalo likiachwa au kuvumiliwa mwisho wa siku linaleta maafa. Wito wangu kwa watu wote ni kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwingine hasa yale makundi ambayo kidesturi yamezoeleka kwamba yananyanyaswa”, ameeleza.