Msanii wa BongoFleva Wini Tz
Wini Tz amesema msanii wa kike anatakiwa apendeze kila wakati asipokuwa na menejmenti au sapoti itampa ugumu kushine ambapo akajitolea mfano kwa kusema aliwahi kununua nywele za gharama ya Milioni 1.
"Kwangu mimi kutongozwa sio changamoto kubwa kwa sababu sijaanza kutongozwa kwenye muziki ila najua jinsi ya kukabiliana na hiyo ishu, kwenye muziki kuna changamoto nyingi kuliko za kutongozwa kwanza wasanii wa kike tuna gharama kuliko wasanii wa kiume, kama anakuwa hana menejmenti au sapoti inakuwa ngumu kwake" amesema Wini Tz
Aidha msanii huyo ameendelea kusema "Vitu ni vingi kwa msanii wa kike anatakiwa apendeze kila wakati ila mimi napendaga kuwa 'natural', kitu cha gharama ambacho niliwahi kununua ni nywele zangu za milioni 1 na laki 2"
Zaidi tazama hapa chini kwenye video

