Wednesday , 2nd Dec , 2020

Katibu mwenezi wa vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Twaha Mwaipaya,amesema wamepanga kutembembea mkoa kwa mkoa kwa ajili ya kuongea na vijana katika kupigania haki na maendeleo ikiwa ni pamoja na kukiimarisha chama. 

Katibu mwenezi wa vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Twaha Mwaipaya

Akizungumza wakati  akikabidhiwa ilani ya sera ambazo watazunguka nazo nchi nzima katika ofisi za makao makuu ya Chama hicho Mwaipaya amesema kuwa  wamejipanga  kuhakikisha jambo hilo linatendeka ambapo pia amedai kuwa wanapambana kwa ajili ya watanzania.

Sambamba na hilo Mwaipaya amedai kuwa ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na wanachama 19 walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu na kudai kuwa yeyote atakayebainika kufanya usaliti atatengwa na chama hicho.

''Sasa nayafurahia mateso ya kukaa gerezani kwa sababu ya watanzania na kupigania haki na kama wanaona usaliti ni njema tutawatenga na aliyezaliwa kwenye chumba cha haki hawezi kuishi kwenye dhuluma’ amesema Twaha Mwaipaya

Aidha Katibu huyo ameongeza kuwa  anayafurahiya mateso hayo ya kukaa gerezani kwa sababu ya watanzania na kudai kuwa wasaliti wote watatengwa na chama hicho