Thursday , 3rd Dec , 2020

Balozi wa Ufaransa nchini Frederic Clavier, amemkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi, barua iliyoandikwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwenda kwa Rais Magufuli, ambaye amempongeza kwa kuiwezesha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati.

Kushoto ni Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Hayo yamejiri mara baada ya Waziri Prof. Kabudi, kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa nchini na kuongeza kuwa baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, kujikita katika uwekezaji mkubwa wa maeneo ya miundombinu na nishati pamoja na huduma za kijamii sasa serikali inalenga kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi.

Tazama video hapa chini