Baadhi ya washtakiwa wakiingia Mahakamani,Kulia ni mshtakiwa Ntemi Masanja na kushoto ni Melaine philippe
Katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Thierry lefeuvre,Melaine philippe raia wa ufaransa,na Ntemi Masanja, ambao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Isaya na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 17,mwaka huu.
Hata hivyo upande wa Utetezi uliowakilishwa na wakili Emmanuel Kessy amesema kuwa mshtakiwa mmoja katika kesi hiyo yupo kwenye mchakato wa kuandika barua ya kuomba kufanya makubaliano ya kukiri kosa yaani "plea bagaining".
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, shtaka la kwanza ni la kuongoza genge la ualifu, shtaka la 2 hadi la 6 ni kushindwa kulipa kodi kati ya Januari 22 mwaka 2019 hadi Julai 19, mwaka 2019 mshtakiwa alishindwa kulipa kodi kwa makusudi kiasi Cha Sh. 1,658,370,376.29 ambayo ni kodi iliyotakiwa kulipwa TRA.
Shtaka jingine la kugushi, Januari 1, 2020 hadi Aprili 2, 2020 mshtakiwa na wenzake watatu wakiwa katika ofisi ya Bevco ltd walitengeneza nyaraka za kuonesha mabadiliko ya hisa katika kampuni iyo pamoja na mabadiliko ya uongozi wakijua kuwa ni uongo.
Pia, mshtakiwa pamoja na wenzake anakabiliwa na kosa la utakatishajia wa fedha alamu kiasi cha Sh. Bilioni 1.6 huku wakijua fedha hizo ni zao la kulipa kodi pamoja na genge la ualifu.Wakilii alidai kuwa ni tarehe tofauti kati ya Julai, 2020.

