Saturday , 5th Dec , 2020

Veronica Lyimo ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo ameitaja siku ya harusi ya rafiki yake kubadili historia ya maisha yake, baada ya kujikuta akishiriki tendo la ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi bila kutumia kinga na ndipo alipojikuta amepata maambukizi.

Veronica Lyimo, anayeishi na Virusi vya Ukimwi

Veronica amesimulia hadithi yake hiyo kwenye kipindi cha MamaMia kinachoruka kila siku za jumatatu hadi Ijumaa kupitia East Africa Radio, ambapo ameeleza kuwa mara ya kwanza kupima UKIMWI ilikuwa mwaka 2015, ambapo vipimo vya awali vilikuwa tata na ndipo alipoamua kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili na ndipo alipoambiwa kuwa tayari ni mwathirika wa VVU.

Veronica anasema kuwa mara baada ya kupokea majibu hayo, alimua kumshirikisha mpenzi wake, lakini mpenzi wake huyo majibu hayo hayakumshangaza kwa kuwa yeye alikuwa akifahamu toka awali kuwa anayo maambukizi.

"Nilipomwambia mpenzi wangu hakushtuka kabisa, kumbe yeye mwenzangu alikuwa anaijua hali yake ya awali kuwa alikuwa na maambukizi, baada ya kupata hayo majibu nililazwa wodi ya vichaa kwa miezi mitatu kwa sababu nilipata sonona, baada ya kutoka mjomba wangu akanichukua na kunipa ushauri nasaha na kunikutanisha na club za vijana wanaoishi na maambukizi", amesimulia Veronica.

Tazama video hapa chini