Saturday , 19th Dec , 2020

Baba yake mzazi na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, Mzee Urban Costa Ndunguru, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 19, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.

Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na kulia ni Baba yake mzazi marehemu Mzee Urban Costa Ndunguru.

Jokate amesema kuwa mzee wake amefikwa na mauti hayo, baada ya kuugua kiharusi na alikuwa amelazwa kwenye chumba cha uangalizi maalum yaani ICU.

Kwasasa taratibu za mazishi zinaendelea. Taarifa zaidi inafuata.