Saturday , 19th Dec , 2020

Wadau Mbalimbali kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa mtaa wa  Mbezi beach B Asha Voniatis, wamejitokeza kufanya usafi pembezoni mwa fukwe lengo ikiwa ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira na kulinda viumbe vilivyopo katika fukwe.

Baadhi ya wadau kutoka Taasisi mbalimbali waliojitokeza kufanya usafi katika fukwe za mbezi B

Wakizungumza na Kurasa hii leo katika zoezi hilo wamesema kuwa athari za utupaji taka hovyo hasa wa chupa za plastiki unahatarisha afya ya binadamu na pia viumbe hai viishivyo baharini.

Nae Dkt.Henry Keneth Njovu,Kaimu Mtendaji ECCT,amesema kuwa uchafuzi wa mazingira ya fukwe ni kutokana na baadhi ya wananchi kutupa taka katika mitaro ambayo baadae husafirisha taka hizo hadi baharini

Ameongeza kuwa madhara ya taka ngumu katika fukwe ni kuharibu viumbe hai katika bahari na kusababisha uchumi kudorora kwani baadhi ya watu wamekuwa wakitegemea uvuvi kujiingizia kipato.