
Jaji mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahimu Juma
Jaji Mkuu ametoa rai hiyo katika hafla ya kuwapokea mawakili wapya 166 ambapo amewataka kusimamia misingi ya haki ili kuisaidia mahakama kufikia maamuzi ya kesi mbalimbali za wateja wao kwa wakati.
''Kwa sasa changamoto ya ajira ni kubwa katika dunia ya ushindani duniani unakuwa kwa kasi teknojia ukichukua nafasi hivyo mawakili hawana budi kupambana na changamoto hii''. Prof Ibrahimu Juma
Aidha amewaonya Mawakili ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uchochezi katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina halisi na wengine majina yasiyo halisi ambao wamekuwa wakikosoa kanuni na sheria zilizowekwa