Monday , 21st Dec , 2020

Mshambuliaji wa Chelsea Timo Werner amesema kuwa ligi kuu ya England ni ngumu kuliko alivyootegemea, lakini anaamini karibu ataonyesha makali yake. Mshambuliaji huyo alijiunga na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu akitokea RB Leipzing ya Ujerumani.

Timo Werner amefunga mabao 4 kwenye michezo 13 ya ligi kuu, tangu ajiunge na Chelsea

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amefunga mabao 4 kwenye michezo 13 ya ligi kuu, tangu ajiunge na Chelsea kwa dau la fedha za uingereza Pauni milion 45 ambayo ni zaidi ya bilioni 138 kwa pesa za kitanzania, akitokea RB Leipzing mwezi Juni.

“Premier League ni tofauti kidogo na ligi niliyotoka. Ni ngumu kuliko vile nilifikiria. Huku mambo ni magumu kuliko Ujerumani, hiki sicho nilichokitarajia. " alisema Werner.

Werner hajafunga goli kwenye michezo 8 ya mwisho kwenye mashindano yote, anasema ratiba ya ligi pia imekuwa ngumu na imechagia kushusha ubora wake.

Timo Werner mwenye umri wa miaka 24 amecheza jumla ya michezo 20 kwenye michuano yote akiwa na kikosi cha Chelsea msimu huu na amefunga mabao 8 yakiwemo mabao 3 kwenye klabu bingwa ulaya na mabao 4 ya ligi kuu.

Na mshambuliaji huyo atakuwa na kibarua cha kuisaidia timu yake kutafuta alama 3 dhidi ya Wes Ham leo usiku katika muendelezo wa ligi kuu nchini England EPL, mchezo utakao chezwa katika dimba la Stanford Bridge. Chelsea imepoteza michezo miwili iliyopita mfululizo.