Sunday , 27th Dec , 2020

Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania (ASFC), kati ya Simba SC dhidi ya Majimaji FC leo, Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara, amewataka wachezaji wasichukulie poa mchezo huo.

Kikosi cha Simba SC kwenye picha kubwa na picha ndogo ni Haji Manara

Manara ameeleza kuwa sababu ya kutochukuliwa poa ni kutokana na misimu miwili nyuma, waliwahi kutolewa na timu ya Green Warriors ya Kigoma, hivyo wachezaji wanatakiwa kujua Simba inataka nini na mashabiki pia wajitokeze kuwapa nguvu wachezaji.

''Wakati tunaiwaza Wida yetu, tusiichukulie poa game yetu ya leo na Majimaji, tujikumbushe misimu miwili nyuma, wachezaji waelewe nini washabiki na Simba inataka na Washabiki waje kutusupport leo na kutuombea'', ameandika Manara.

Disemba 23, 2017 klabu ya Green Warriors ambayo ilikuwa inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania iliitoa Simba SC kwenye michuano hiyo baada ya kutoka saree ya 1-1 ndani ya dakika 90 kisha kushinda kwa penati 4-3.

Mechi nyingine za leo ni kati ya Namungo FC ambao wanacheza na wababe hao wa Simba mwaka 2017, Green Warriors huku Mtibwa Sugara wakicheza na Geita Gold.