
Kulia ni Harmonize kushoto ni Hamis Bss
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Hamis Bss amefika mbali zaidi kwa kusema kama msanii huyo amemkosea basi anaomba amsamehe kwani mwanzo alionesha nia ya kutaka kumsapoti wakati alipokuwa kwenye mashindano.
"Ningeomba sana anisaidie, ujue mpaka mtu anafikia hatua ya kulia kwa ajili ya kuomba msaada sio poa, anisadie kwa chochote kile hata kwa wimbo mmoja au video tu kwa sababu anajuana na watu wengi, alivyosemaga kwamba atanisaini na kunisaidia nilidhani nimeshatoboa au kama nimemkosea naomba anisamehe" ameeleza Hamis
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.