Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TAKUKURU yabaini wizi mpya wa dawa MOI

Wednesday , 13th Jan , 2021

Watumishi 23 wa Kitengo cha Famasia cha Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma za kuandika taarifa za uongo katika mfumo wa utunzaji taarifa za kumbukumbu za utoaji dawa na vifaa tiba,

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,  Brigedia Jenerali John Mbungo.

na kusababisha upotevu wa dawa zenye thamani ya shilingi bilioni 1.2.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari, 13, 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,  Brigedia Jenerali John Mbungo, wakati anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa watumishi hao wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kati ya mwaka 2018 hadi 2020.

Akielezea namna ubadhirifu huo ulivyofanyika, Brigedia Mbungo amesema watuhumiwa hao walikuwa wanaandika taarifa za uongo katika mfumo huo, kwa kuweka idadi kubwa ya vifaa vilivyotolewa tofauti na idadi halisi iliyotolewa kwa wateja na madaktari.

"TAKUKURU kwa kushirikiana na MOI imedhibiti uchepushaji na ubadhirifu wa madawa ya zaidi ya Tsh Bil. 1.2, ambazo zilihujumiwa kwa manufaa binafsi na watumishi wa kitengo cha famasia katika taasisi hiyo"amesema Brigedia Mbungo.

Brigedia Mbungo  ameongeza kuwa, "Ubadhirifu huu umebainika kutokana na uwepo wa tofauti kati ya taarifa za dawa zilizoingizwa na wafamasia na zile zilizoandikwa na madaktari ikilinganishwa na fomu za wagonjwa zilizotoa maelekezo ya aina ya dawa".

Brigedia Mbungo amesema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na kwamba mahojiano yakikamilika hatua za kisheria zitafuatwa.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine