Wednesday , 13th Jan , 2021

Zoezi la ukataji wa tiketi kielektroniki kwa abiria wa mabasi yaendayo mikoani, imetajwa kama moja ya changamoto kubwa itakayopoteza ajira kwa mamia ya vijana nchini hasa waliokuwa wakikatisha tiketi hizo kwa kuandika.

Mmoja ya wakatisha tiketi kielektroniki Adam Suleiman akimpatia maelekezo abiria katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

EATV imefika katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam kushuhudia namna utekelezaji wa Teknolojia hiyo unavyoendelea na kukutana na malalamiko kutoka kwa watendaji wa maeneo hayo.

Uelewa mdogo kwa abiria imekuwa chanzo cha migogoro ya ukataji tiketi kielektroniki, abiria hajui kama kufanya ‘booking’ sio kukata tiketi akikuta tiketi imeuzwa analalamika”, amesema Nassib Dello mmoja wa Mfanyakazi kituo cha mabasi Ubungo.

Sanjari na hayo suala la Elimu ya ukataji tiketi kwa njia ya mtandao kwa abiria umetajwa kuwa changamoto pia kutokana na changamoto za kimtandao.